Klabu ya Kariobangi Sharks inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya imethibitisha kuwa itakuja nchini August 04 kwenye mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi
Mabingwa hao wa kombe la SportPesa ambao hivi karibuni waliweka rekodi ya kuifunga Everton huko Kenya, kupitia ukurasa wao wa mtandao wa Twitter, wamethibitisha watakuja nchini kucheza na Yanga August 04
"Tunafuraha tele kama klabu kuthibitisha ya kuwa tumekubali mualiko kutoka rafiki zetu Yanga kutoka Tanzania, kushiriki katika mechi ya kirafiki itakayo chezwa Agosti 04 mjini Dar es Salaam, kusheherekea Tamasha la Wiki ya Mwananchi," imesema taarifa ya timu hiyo
Yanga itatumia mchezo huo kutambulisha kikosi chake pamoja na jezi za msimu wa 2019/20
Kabla ya mchezo huo, kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo michezo miwili ya kirafiki kati ya wasanii wa bongo muvi na bongo fleva na mchezo kati ya wakongwe wa Yanga dhidi ya wenzao wa Pamba Fc