March 06 2018, Yanga ilicheza na Township Rollers katika mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Taifa, uliwashuhudia mabingwa hao wa kihistoria wakikubali kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo ambao 'waliburuzwa' kwelikweli
Hata hivyo wakati huo Yanga ilikumbana Rollers ikiwa katika wakati mgumu sana wa kiuchumi
Kwa kiasi kikubwa kipigo hicho cha nyumbani kilitokana na maandalizi 'hafifu' kutokana hali mbaya iliyokuwa ikiikabili timu
Hebu tujikumbushe kikosi kilichoanza kwenye mchezo huo;

Kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa Botswana, Yanga 'ilikomaa' na kulazimisha suluhu ya bila kufungana
Yanga ikatolewa kwenye mashindano na kutupwa michuano ya kombe la Shirikisho ambako walifanikiwa kutinga hatua ya makundi baada ya kuiondosha Welayta Dicha kwa kuichapa 2-0 nyumbani na kupoteza 1-0 ugenini
Lakini mwaka huu mambo yatakuwa tofauti sana kwani Rollers watakutana na mziki mwingine kabisa
Katika kikosi kilichoanza mwaka jana, ni wachezaji wawili tu Yondani na Tshishimbi ambao bado wako kikosini na huenda wakawemo kwenye kikosi kitakachoikabili timu hiyo August 09,10 au 11 jijini Dar es salaam
cutYanga itakuwa na mabadiliko makubwa kwenye safu yake ya ulinzi, kiungo na watakuwa na safu mpya kabisa ya ushambuliaji
Walinzi wapya Lamine Moro, Ally Mtoni, Mustafa Suleyman na Ally Ally wameimarisha eneo hilo ambalo wakati huo liliwategemea zaidi Yondani na Dante
Wakati huo Yanga ilikuwa ikitegemea mshambuliaji mmoja tu mbele, Obrey Chirwa lakini sasa ina washambuliaji hatari Ladney Urikhob, Maybin Kalengo na Juma Balinya
Ambao watasaidiwa na viungo mahiri wa pembeni akina Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Mrisho Ngasa na Deus Kaseke
Kiungo cha kati kiko imara sana sasa kwani pamoja na uwepo wa Tshishimbi, akina Mapinduzi Balama, Feisal Salum, Raphael Daudi na Abdulaziz Makame wameongeza uimara katika eneo hilo
Langoni sasa hakuwa wasiwasi tena ujio wa Farouk Shikalo na Metacha Mnata umemaliza kabisa changamoto iliyokuwa ikikabili eneo hilo
Hawa Rollers inapaswa wajiandae kisaikolojia kwani kama bado wanaifikiria Yanga ile ambayo langoni alikuwa Kabwili, wanaweza kuondoka hapa na kapu la mabao
Aidha hii ni nafasi pia kwa Yanga kulipa kisasi kwa Wabotswana hao
Yanga ina nafasi ya kutinga hatua ya makundi kwani kama itaiondosha Township Rollers, itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Green Mamba ya Eswatini dhidi ya ZESCO United inayonolewa na aliyekuwa kocha wa Yanga, George Lwandamina