Yanga hii anayetoka moto anayeingia moto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jul 2019
Yanga hii anayetoka moto anayeingia moto

Yanga inajifua mkoani Morogoro ikiendelea na maandalizi ya msimu ya msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara pamoja na michuano mbalimbali

Hata hivyo tayari wachezaji wa timu hiyo wameanza kuzungumzia jinsi ushindani wa namba unavyoanza kushamiri kwenye kikosi cha timu hiyo

Kwa jinsi Yanga ilivyofanya usajili wake, karibu kila nafasi ina wachezaji wawili ambao wana sifa ya kuanza kikosi cha kwanza

Hali hiyo ndio inayofanya kuongezeka kwa ushindani hata mazoezini kwani kila mchezaji anataka kujihakikishia nafasi mapema

Wakati msimu uliopita Yanga ilimtegemea mshambuliaji mmoja, msimu huu hali inaweza kuwa tofauti kutokana na ujio wa washambuliaji Sadney Urikhob, Juma Balinya na Maybin Kalengo

Washambuliaji hao wote wameonyesha uwezo mkubwa mazoezini na hakika watampa kazi Zahera ya kuamua nani aanze

Safu ya kiungo pia ushindani umekuwa mkubwa kutokana na ujio wa Mapinduzi Balama, Abdulaziz Makame wakiwa ni viungo wa kati wakati Issa Bigirimana na Patrick Sibomana wakiwa ni viungo wanaotokea pembeni

Hawa wanaungana na waliokuwepo Papi Tshishimbi, Feisal Salum, Raphael Daudi, Mrisho Ngasa na Deus Kaseke huku kinda Gustafa Simon akiongezeka katika eneo hilo

Ujio wa wachezaji wapya umeonekana kumuimarisha zaidi Ngasa ambaye moto wake huko Morogoro hauzimiki!

cut

Safu ya ulinzi ndio inaweza kuwa na ushindani zaidi kwani ukiondoa nafasi za ulinzi wa pembeni ambazo Boxer na Marcelo wanaweza kuwa wamejihakikishia, kati shughuli itakuwa pevu

Mkongwe Kelvin Yondani, Ally Ally, Lamine Moro, Ally Mtoni, Cleofas Sospeter, Andrew Vicent na Mustapha Suleyman wote watakuwa wakiwania nafasi mbili za ulinzi wa kati

Ahueni itakuwa kwa Mtoni na Chikupe ambao wanaweza kucheza pembeni

Langoni nako, licha ya Farouk Shikalo kuwa katika nafasi nzuri, Metacha Mnata atakuwa karibu kuchukua nafasi yake kama atafanya makosa

Msimu huu Yanga haitakuwa na changamoto langoni kwani imesajili magolikipa wanne

Ushindani wa namba utainufaisha zaidi Yanga kwani kila mchezaji atakayepata nafasi kwenye kikosi cha kwanza atalazimika kufanya kazi ya ziada kuilinda nafasi hiyo

Kwani kosa moja tu linaweza kumuondoa kikosini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’