Boxer afurahia kuitwa Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jul 2019
Boxer afurahia kuitwa Stars

Beki Paulo Godfrey 'Boxer' amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambacho Julai 28 kitaumana na Kenya katika mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za CHAN kwa wachezaji wanaocheza ndani

Kocha Etinne Ndayiragije amefanya uamuzi sahihi wa kumjumuisha beki huyo mwenye kasi ambaye alin'gara zaidi kwenye ligi kuu msimu uliopita

Wengi wanaamini angeweza kujumuishwa hata kwenye kikosi kilichokwenda Misri kushiriki michuano ya Afcon

Wito huo umemuongezea ari Boxer ambaye kipaji chake kiliibuliwa na kocha Mwinyi Zahera aliyempandisha kutoka timu ya vijana ya Yanga kuchukua nafasi ya Hassani Kessy aliyetimkia Nkana Fc

"Nimefurahi kuitwa timu ya Taifa..nashukuru kocha ameniamini na nitaitumia nafasi hiyo kuipigania nchi yangu," amesema

"Pia nawashukuru benchi la ufundi la Yanga kwani wamenisaidia mpaka leo naweza kupata nafasi hii"

Hii mara ya kwanza kwa Boxer kujumuishwa kwenye timu ya wakubwa. Aliitwa kwenye kikosi cha U23 ambacho kilicheza na Burundi mwaka jana

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’