Uongozi wa Yanga umesema tayari umewasiliana na klabu ya Bandari Fc ili kumaliza sintofahamu iliyojitokeza kuhusu mlinda lango Farouq Shikalo
Bandari Fc ilipinga usajili wa Shikalo kutua Yanga wakidai kuwa mlinda lango huyo bado ana mkataba
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema suala hilo linashughulikiwa na hakuna jambo litaharibika
Jana Shikalo alinukuliwa na mtandao wa GOAL akisema kuwa bado hajasaini mkataba wa kuitumikia Yanga, kilichopo ni mazungumzo tu
Hata hivyo kauli hiyo aliitoa kutokana na sintofahamu iliyojitokeza, lakini tayari Shikalo amemalizana na Yanga na hakuna shaka atawatumikia mabingwa hao wa kihistoria msimu ujao
ADVERTISE HERE