Uongozi wa Bandari Fc umesema mlinda lango Farouq Shikalo aliyesajiliwa na Yanga bado ana mkataba na klabu hiyo
Shikalo alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga akiwa Misri na timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars

Bandari imesisitiza kuwa Shikalo bado ni kipa wao kwa kuwa mkataba wake haujamalizika
Uongozi wa Yanga utalazimika kumalizana na Bandari Fc ili kuweza kupata uhamisho wake wa Kimataifa aweze kuitumikia Yanga
La sivyo Yanga haitaweza kumtumia Shikalo mpaka mkataba wake utakapomalizika
Bandari Fc wanasema mkataba wake unamalizika mwezi wa 12
Sintofahamu kama hii pia ilitokea kwa kiungo Issa Bigirimana ambaye klabu yake ya APR ilidai alisajiliwa na Yanga huku akiwa na mkataba
Hata hivyo Bigirimana alimalizana na APR mwenyewe na kupewa baraka zote kuitumikia Yanga