Changamoto inayoikabili Yanga sasa ni kuanza maandalizi ya msimu mpya bila ya kuwa na kocha wake Mkuu Mwinyi Zahera ambaye yuko Misri na timu ya Taifa ya DR Congo akishiriki michuano ya Afcon
Zahera anaweza kuchelewa kurudi kama DR Congo itafanikiwa zaidi kwenye michuano hiyo hasa kama itafuzu hatua ya nusu fainali na hata fainali
Kutokana na kikosi cha Yanga kujaa nyota wengi wapya, ilipaswa Zahera mwenyewe aifanye kazi ya kukiandaa kikosi chake tangu mwanzo
Ikumbukwe michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu itaanza mapema mwezi wa nane, kama Zahera atarejea mwishoni mwa mwezi ni dhahiri atakuwa na siku chache za kuiandaa timu
Viongozi wa Yanga walipaswa kuliangalia hili kwa mapana ili kocha huyo apewe mkataba ambayo utamuondolea majukumu ya timu ya Taifa
Licha ya kuandaa program ya mazoezi na kumuachia Mwandila, lakini naamini mafanikio zaidi yangepatikana kama angesimamia mazoezi hayo yeye mwenyewe