Kama migomo imeanza mapema hivi, mungu atusaidie

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Sep 2017
Kama migomo imeanza mapema hivi, mungu atusaidie
Uongozi wa Yanga umekanusha juu ya mgomo wa wachezaji jana na kusisitiza mazoezi yaliahirishwa kupisha kikao cha wachezaji na viongozi wa timu.

Wachezaji wamefanya mazoezi leo katika dimba la Uhuru baada kikao hicho kufanyika jana.

Hata hivyo huenda kikao hicho kiliitishwa baada ya wachezaji kulalamika kuhusu hatma ya mishahara yao ikidaiwa kuwa hawajalipwa kwa miezi miwili pamoja na posho za mechi.

Wakati matarajio ya kila MwanaYanga kuwa msimu huu ni kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo, ni wazi yanaweza yasifanikiwe kama matatizo haya hayatapatiwa ufumbuzi haraka.

Mfumo wa utegemezi umeiathiri Yanga kwa kiasi kikubwa na viongozi wanahitaji pongezi kwa juhudi zao za kuongeza vyanzo vya mapato ili timu ijitegemee.

Juhudi hizo zifanyike haraka ili kuondoka na 'aibu' hii ya migomo ya wachezaji kwani ina athari ya moja kwa moja kwa mafanikio ya timu.

Wachezaji hawapaswi kulaumiwa kwa matukio haya kwani wanadai haki yao. Naamini mpaka wanafikia kugoma basi wamevumilia ahadi kadhaa.

Hii ni changamoto kwa WanaYanga wote na hapaswi kulaumiwa yeyote. Timu hii ni ya Wananchi wakati ule Manji analipa mishahara ya wachezaji ilikuwa kwa sababu ya mapenzi yake makubwa kwa klabu ya Yanga.

Sasa ni wakati wa WanaYanga kuisadia timu yao sio kwa pesa tu, bali na mawazo ya kumaliza kabisa utegemezi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’