Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amewaomba watanzania kuichangia timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambayo ipo Misri kwa ajili ya michuano ya AFCON 2019
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Dk Mwakyembe amesema siku ya Alhamisi Harambee maalum ya kuichangia timu hiyo itafanywa
"Siku ya Alhamisi asubuhi tutakuwa na zoezi kubwa ambalo litaluwa LIVE kwenye mitandao na television mbalimbali na kwenye radio ambapo tutafanya uchangiaji wa Taifa Stars."
"Nawahakikishia kila shilingi itakayopatikana itakwenda kwa vijana wetu, wasishindwe kwa kuvunjika moyo."
Dk Mwakyembe amesema, fedha hizo zinazochangishwa ni kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji
"Fedha zitakazochangwa si kwa ajili ya kuipeleka timu Misri na kuirudisha, hatuhitaji kuwaweka kwenye hotel nzuri (hayo yote yameshafanyika, tunahitaji kuwapa motisha wachezaji ili waweze kufanya vizuri"