Balinya asaini miaka miwili Yanga, kaletwa Dar na Simba, kilichotokea..

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jun 2019
Balinya asaini miaka miwili Yanga, kaletwa Dar na Simba, kilichotokea..

Mshambuliaji wa Polisi Fc ya Uganda Juma Balinya jana alikamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili

Mfungaji bora huyo wa ligi kuu ya Uganda msimu uliomalizika, alikamilisha usajili kabla ya kutambulishwa rasmi na Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela kwenye tukio la Harambee ya kuichangia Yanga maarufu kama Kubwa Kuliko

Hata hivyo Balinya ilikuwa asajiliwe na Simba na inaelezwa alitarajiwa kutambulishwa jana saa saba mchana

Inaelezwa Simba ndio iliyogharamia ujio wa mshambuliaji huyo kutoka Uganda hata hivyo Yanga ikauteka mchakato na kumalizana nae 'juu kwa juu' na kuwaacha watani zao wakiwa wameduwaa wasijue cha kufanya

Usajili wa Balinya hautofautiani sana na usajili wa Abdulaziz Makame ''Bui' ambaye alisajiliwa na Yanga huku mkononi akiwa na nauli ya boti aliyokuwa ametumiwa na viongozi wa Simba!

Kilichotokea, Yanga walimtumia tiketi ya ndege wakati akijiandaa kwenda kupanda boti ambapo inaelezwa viongozi wa Simba walikuwa Bandarini wakisubiri kumpokea

Balinya na Bui wote walitambulishwa jana ukumbi wa Diamond Jubilee kwenye Kubwa Kuliko

Uongozi wa Yanga umetamba kuwa mpaka sasa wamewazidi ujanja wapinzani wao kwa kuwasajili wachezaji hao wakati Simba haikusajili mchezaji hata mmoja ambaye alikuwa kwenye mipango ya Yanga

Mlindalango Beno Kakolanya amesajiliwa na Simba lakini tayari Yanga walikuwa wameachana nae mwingine anayesubiri kutambulishwa ni Ibrahim Ajib ambaye pia Zahera amesisitiza hayumo kwenye hesabu zake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’