Zahera afichua siri ya kumpa Ajib unahodha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jun 2019
Zahera afichua siri ya kumpa Ajib unahodha

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amefichua uamuzi wa kumpa unahodha kiungo Ibrahim Ajib aliufanya ili kumsaidia ajitambue na hatimaye kuwa na mchango katika klabu ya Yanga

Amesema baada ya kutambua kipaji cha kiungo huyo alimpa majukumu ya uongozi wa wenzie ili kumuongezea nidhamu na kumfanya aweze kufika mbali

Hata hivyo Zahera amesema alikata tamaa na Ajib baada ya kukataa kujiunga na TP Mazembe ili aendelee kubaki hapa nchini

"Nilimpa unahodha ili kumuongezea nidhamu ya soka na utambuzi ili aweze kufika mbali," amesema

"Nilijua akiwa nahodha atakuwa karibu na mimi nami nitaendelea kuweka juhudi na bidii kwake kama injini ya timu ili afike mbali"

"Naweza kuwa nimefanikiwa kwa kiasi kidogo, kwa ujumla Ajib sio mchezaji mbaya"

"Ajibu ni mchezaji mzuri ila bado hajajitambua yeye ni nani katika soka"

"Alivyoniambia amepata ofa Mazembe nilifurahi sana lakini baadae nikaskia mara amesinya Simba mara anaonekana Ndondo Cup hapo ndipo sikumuelewa"

"Mchezaji akishakosa muelekeo wa soka lake ni ngumu sana kujivunia mafanikio kwenye ulimwengu wa soka"

"Sifa kuu ya mchezaji ni kutambua yeye ni nani katika soka, Nafasi yake katika soka, Nini malengo yake katika soka, Na kwanini amechagua soka na si music or fashion??!"

"Kumkataa Ajibu sio kwamba ni mbaya ila nataka ajitambue, na ili kujitambua acheze nje ya Yanga ili nione kujitambua kwake"

Ajib tayari ameshakamilisha usajili wa kujiunga na Simba ambapo inaelezwa timu hiyo itamtambulisha Julai 01 baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika Juni 30

Zahera amesema alimuondoa Ajib kwenye mipango ya kikosi chake cha msimu ujao baada ya kinara huyo wa pasi za mabao kupata ofa kutoka TP Mazembe

Amesema hata baada ya Ajib 'kuipotezea' ofa ya Mazembe, hakutaka asajiliwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’