Sitaingilia majukumu ya Zahera - Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 May 2019
Sitaingilia majukumu ya Zahera - Dk Msolla

Licha ya kuwa na taaluma ya ukocha Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amemuhakikishia kocha Mwinyi Zahera kuwa hatamuingilia kwenye majukumu yake

Dk Msolla ana taaluma ya ukocha na aliwahi kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

"Nimezungumza na kocha kuhusu hili. Nimemuhakikishia awe huru kutekeleza majukumu yake," amesema

"Nitajikita zaidi katika uongozi kuhakikisha yale niliyoyaahidi wakati wa kampeni tunayatekeleza"

"Tutampa Zahera ushirikiano wote atakaohitaji, na kama atahitaji ushauri wa kiufundi kutoka kwangu basi nitampatia"

Katika hatua nyingine Dk Msolla amesema wameanza mkakati wa kuongeza wanachama kwa kuanzisha matawi mapya

cut

"Tunataka tuhamasishe sana uanzishwaji wa matawi mapya nchi nzima," amesema

"Tutaigawa mikoa kwenye kanda ambapo kila kanda tutapeleka Mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji, mchezaji mmoja wa zamani na mchezaji mmoja anayecheza sasa"

"Tutahakikisha wanapita kina kona ya nchi kushawishi mashabiki wawe wanachama"

Aidha Dk Msolla amesema wataongeza ushiriki wa wanachama katika kufanya maamuzi ya timu hiyo kupitia teknolojia kwa kuwashirikisha hukohuko waliko

Utaratibu wa sasa unawapa zaidi fursa wanachama wa jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’