Ten awaaga Makambo, Ajib amkaribisha Koukpo 'kiaina'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 May 2019
Ten awaaga Makambo, Ajib amkaribisha Koukpo 'kiaina'

Heritrier Makambo na Ibrahim Ajib wamebakisha wiki moja tu ya kuitumikia Yanga kwani baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc, wachezaji hao hawatakuwa mali ya Yanga

Wakati Makambo akisubiri kutimkia Horoya AC, Ajib anaelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kujiunga na mabingwa wa nchi hiyo, TP Mazembe

Afisa Habari wa Yanga Dismas amewatakia kila la kheri wachezaji hao waliokuwa na mchango mkubwa kwa kikosi cha Yanga msimu huu

Wakati Makambo akifunga mabao 17, Ajib amehusika katika mabao 23, akitengeneza 17 na kufunga sita

Ten amesema wawili hao wangetengeneza 'combination' ya hatari na Marcellin Koukpo ambaye anatajwa kusajiliwa na Yanga

"Simba kuna utatu wa Kagere, Bocco na Okwi nawaza sijui ingekuwaje kama nasi tungepata utatu wa Ajib,Β  Makambo na Koukpo"

"Simaanishi kwamba waliokuwepo hawawezi, lakini wakati mwingine si vibaya kuwaza kwa mafanikio ya mwingine. Kikubwa kila timu ijenge kikosi imara ili tuwe na ligi ya ushindani kweli mwakani" amendika Ten kwenye ukurasa wake wa Instagram

cut

Yanga itamkumbuka Ajib kwa mchango wake aliotoa kwa klabu hiyo tangu alipojiunga kutoka Simba misimu miwili iliyopita, wakati Makambo amecheza Yanga kwa msimu mmoja lakini atakumbukwa kwa uhodari wake wa 'kuzijaza' mabao timu pinzani

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ana kazi ya kusaka wachezaji watakaoziba nafasi zao.

Mwenyewe amewatoa hofu mashabiki wa Yanga akiwahakikishia kuwa atasajili wachezaji wenye uwezo sawa au zaidi yao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’