Mshambuliaji wa Azam Fc Obrey Chirwa amegoma kusaini mkataba mpya kunako klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu
Azam Fc imekuja na utaratibu tofauti wa kuwaongezea mikataba wachezaji wake kabla ya mikataba yao ya awali kumalizika
Timu hiyo tayari imewapa mikataba wachezaji wake waandamizi isipokuwa Chirwa aliyejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miezi sita wakati wa dirisha dogo la usajili
Hivi karibuni kocha Mwinyi Zahera alieleza kuvutiwa na kiwango cha mshambuliaji huyo raia wa Zambia
Zahera alisema Chirwa ni bonge la mchezaji, lakini alikataa kuweka wazi kama anaweza kumrejesha tena kikosini kwa ajili ya msimu ujao
Alitaja hali ngumu ya kiuchumi Yanga ilikuwa sababu ya yeye kukataa asisajiliwe aliporejea kutoka Misri mwishoni mwa mwaka jana
"Chirwa ni mchezaji mkubwa na anapambana sana katika uchezaji wake hata kwa mechi nilizomuona ana kitu ambacho wengine hawana, ila nilimkataa kwa kuwa hawezi kuvumilia matatizo," alisema
Hata hivyo kama Yanga itafanikiwa kukusanya kiasi cha pesa kilichokusudiwa, msimu ujao huenda isiwe na changamoto ya kulipa mishahara ya wachezaji
Wakati huohuo uongozi wa timu hiyo chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla, umeahidi kukamilisha mchakato wa kubadili mfumo wa uendeshaji wa Yanga ndani ya mwaka mmoja
Huenda Chirwa akawa na nafasi ya kurejea Yanga hasa ikizingatiwa mwenyewe ameonyesha kuwa na mapenzi makubwa na Yanga
Wakati huu ambao Yanga inamuuza Heritier Makambo, Chirwa ni mshambuliaji ambaye anaweza kuchukua nafasi yake pia anaweza akatafutiwa mshambuliaji mwingine mwenye makali zaidi yake
Yanga inahitaji kurudisha makali yake ya kuzifumania nyavu msimu ujao kwa kuboresha safu yake ya ushambuliaji