Mlinzi wa kati kutoka klabu ya SM Sanga Balende inayoshiriki ligi kuu nchini DRC, Fiston Kayembe yuko kwenye kikosi cha Yanga wiki ya pili sasa akifanya majaribio.
Mchezaji huyo alipendekezwa na kiungo Papi Kabamba Tshishimbi ambaye pia ni raia wa Congo.
Tayari mlinzi huyo ameonyesha makeke yake na amemkuna kona George Lwandamina na hakuna shaka huyu atasajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Novemba.
Mkataba wa Kayembe na klabu yake ya SM Sanga unamalizika mwishoni mwa mwezi huu hivyo ni wazi Yanga haitakumbana na vikwazo kupata sahihi yake.
Lwandamina amemwagia sifa mlinzi huyo kuwa ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kupiga pasi, kucheza mipira ya juu na chini sambamba na mambo mengine ya msingi.
“Ni mchezaji makini, nimemtazama kwa muda ambao tumekuwa hapa na kugundua kuwa ana kitu cha tofauti,†alisema Lwandamina.
“Ana maamuzi sahihi pia ya kufahamu kipi afanye kwa wakati husika.
“Mpaka sasa naweza kusema amefikia matarajio yangu. Kama unavyofahamu tuna mashindano ya kimataifa na tunahitaji mtu ambaye atakuwa na kitu cha tofauti, nimekiona kwake.â€
Kayembe ni mchezaji wa nne kufanya majaribio kwenye kikosi cha Yanga kinachosaka mahiri atakayemalizia nafasi moja ya mchezaji wa Kimataifa.

ADVERTISE HERE