Kwa huyu Mcongo Bossue mtamsahau

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
14 Sep 2017
Kwa huyu Mcongo Bossue mtamsahau
Mlinzi wa kati kutoka klabu ya SM Sanga Balende inayoshiriki ligi kuu nchini DRC, Fiston Kayembe yuko kwenye kikosi cha Yanga wiki ya pili sasa akifanya majaribio.

Mchezaji huyo alipendekezwa na kiungo Papi Kabamba Tshishimbi ambaye pia ni raia wa Congo.

Tayari mlinzi huyo ameonyesha makeke yake na amemkuna kona George Lwandamina na hakuna shaka huyu atasajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Novemba.

Mkataba wa Kayembe na klabu yake ya SM Sanga unamalizika mwishoni mwa mwezi huu hivyo ni wazi Yanga haitakumbana na vikwazo kupata sahihi yake.

Lwandamina amemwagia sifa mlinzi huyo kuwa ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kupiga pasi, kucheza mipira ya juu na chini sambamba na mambo mengine ya msingi.

“Ni mchezaji makini, nimemtazama kwa muda ambao tumekuwa hapa na kugundua kuwa ana kitu cha tofauti,” alisema Lwandamina.

“Ana maamuzi sahihi pia ya kufahamu kipi afanye kwa wakati husika.

“Mpaka sasa naweza kusema amefikia matarajio yangu. Kama unavyofahamu tuna mashindano ya kimataifa na tunahitaji mtu ambaye atakuwa na kitu cha tofauti, nimekiona kwake.”

Kayembe ni mchezaji wa nne kufanya majaribio kwenye kikosi cha Yanga kinachosaka mahiri atakayemalizia nafasi moja ya mchezaji wa Kimataifa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
58m ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE →