Lwandamina aachwe afanye kazi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2017
Lwandamina aachwe afanye kazi
Ligi kuu msimu huu ndio kwanza imeanza sasa inaelekea mzunguuko wa tatu ambapo Jumamosi ijayo Septemba 16 Yanga itakuwa ugenini ikichuana na Majimaji mkoani Ruvuma.

Yanga ina alama nne baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja.

Ukiangalia msimamo wa ligi baada ya michezo miwili, Mtibwa Sugar ndio inaongoza ikiwa imejikusanyia alama sita. Simba, Prisons, Lipuli, Yanga na Azam zote zina alama nne zinatofautiana kwa mabao tu.

Licha ya Yanga kuwa miongoni mwa timu ambapo hazijapoteza mchezo kuna baadhi ya mashabiki wanalalamika kuwa kocha George Lwandamina hafai na hataisaidia Yanga kutwaa taji msimu huu.

Maoni ya wengi ni kuwa kocha hana mbinu za kuiwezesha Yanga kutwaa ubingwa licha ya kuwa na kikosi bora.

Wamesahau ni huyu huyu Lwandamina anayeambiwa hana mbinu aliiwezesha Yanga kutwaa taji la tatu mfululizo akiwa kwenye mazingira magumu.

Ikumbukwe msimu uliopita Lwandamina aliichukua Yanga kutoka mikononi mwa kocha Hans van Pluijm ikiwa na matatizo lukuki.

Majeruhi, wachezaji kugoma mara kadhaa kutokana na kutolipwa mishahara kwa miezi hadi mitatu. Kuna kipindi Yanga ilikuwa nyuma ya Simba kwa tofauti ya alama tisa lakini ikafanikiwa kutwaa ubingwa.

Ni vyema mashabiki wakawa na utamaduni wa kuwa na timu kwenye mazingira yote.

Inafahamika mwanzoni mwa msimu huu Lwandamina amewakosa wachezaji wake muhimu kutokana na sababu mbalimbali. Obrey Chirwa, Amissi Tambwe na Simon Msuva ndiyo waliipa Yanga ubingwa msimu uliopita.

Msuva amekwenda Morocco, Chirwa ndio kwanza amerejea dimbani wiki iliyopita huku Tambwe akiwa bado majeruhi.

Ni dhahiri Lwandamina alikuwa amejenga kikosi chake kuwategemea Msuva, Tambwe na Chirwa kupata mabao lakini sasa analazimika kubadili mfumo kulingana na wachezaji waliopo.

Msuva, Tambwe na Chirwa waliifungia Yanga jumla ya mabao 37 msimu uliopita. Kukosekana kwao lazima kuiathiri Yanga katika upachikaji mabao.

Wote tunakubaliana Yanga haikuweza kuziba pengo la Msuva wakati wa dirisha la usajili. Huyu Msuva alichangia asilimia 80 ya mabao ya Yanga msimu uliopita. Iwe kwa kutengeneza au kufunga mwenyewe.

Ni kweli usiopingika kwamba wachezaji waliopo ambao wanacheza nafasi ya Msuva hakuna aliyemkaribia mkali huyo ambaye sasa anakipiga na Difaa El Jadida.

Kocha analazimika kubadili mbinu na atahitaji muda kujua mbinu gani atumie kuiwezesha timu ishinde bila ya Msuva.

Licha ya kwamba Yanga ina wachezaji mahiri kama Ibrahim Ajib na Donald Ngoma lakini bado wawili hao hawajaonyesha makali yao na wanahitaji muda.

Ngoma alikaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha ni dhahiri ameathiriwa kwa kiasi fulani. Ngoma huyu tuliyemuona kwenye michezo kadhaa ya Yanga msimu huu sio yule tunayemfahamu. Je ni kosa la kocha pale mchezaji anapocheza chini ya kiwango?

HITIMISHO

Ni mapema sana kuanza kumlaumu kocha. Aachwe afanye kazi yake tusubiri baada ya michezo hata mitano tuone atakuwa amefanikiwa kwa kiasi gani.

Kwa sasa Yanga inafanya vizuri, na Habari njema ni kwamba muda si mrefu wachezaji wote waliokuwa majeruhi watakuwa kikosini.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’