Kesho Yanga itakuwa na nafasi ya kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kama itapata ushindi dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamika ambapo wachezaji wako katika hali nzuri isipokuwa wachezaji watatu ambao ni majeruhi na wataukosa mchezo huo
Mohammed Issa, Gadiel Michael na Andrew Vicent Chikupe watakosekana kesho kutokana na kusumbuliwa na majeraha
Nahodha Ibrahim Ajib aliyekosa mchezo dhidi ya Biashara United kutokana na maradhi, huenda akarejea kikosini kesho
Matokeo ya 0-0 iliyopata Simba dhidi ya Azam Fc leo yanaipa nafasi Yanga kuongoza ligi kesho kama itashinda
Yanga inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 80 wakati Simba imefikisha alama 82 baada ya kulazimishwa suluhu leo