Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema amepokea barua ya mashitaka kutoka Bodi ya ligi akitakiwa kujieleza juu ya tuhuma mbalimbali anazotoa kutokana na uendeshaji wa ligi kuu
Hata hivyo amesema hataacha kuzungumza pale anapoona makosa yanafanyika
Zahera amewavaa waamuzi waliochezesha mchezo wa jana dhidi ya Biashara United kwa kukubali bao ambalo mfungaji alikuwa ameotea
"Bodi ya ligi walinitumia barua wakitaka nikajieleze. Lakini nimesema sitaacha kuzungumza pale ninapoona timu yangu haitendewi haki. Angalia lile bao walilotufunga Biashara lilikuwa sahihi? Hii ni aibu kwa mtindo huu soka la Tanzania haliwezi kuendelea"
Zahera ni miongoni mwa makocha watatu wa timu zinazoshiriki ligi kuu walioitwa kujieleza Kamati ya Nidhamu ya TFF kutokana na tuhuma mbalimbali walizotoa
Makocha walioitwa ni Athuman Bilal wa Stand United, Mwinyi Zahera (Yanga), Nassoro Mrisho (Geita Gold FC), na Ramadhani Nsanzurwimo (Mbeya City).