Ninja, Chikupe wawatuliza Chirwa na Ngoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Apr 2019
Ninja, Chikupe wawatuliza Chirwa na Ngoma

Washambuliaji wa zamani wa Yanga Obrey Chirwa na Donald Ngoma ambao wanakipiga katika klabu ya Azam Fc leo wameshindwa kufurukuta mbele ya waajiri wao wa zamani wakikubali kipigo cha bao 1-0

Walinzi wawili wa kati wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' na Andrew Vicent 'Dante' leo walikuwa na kazi maalum ya kuhakikisha washambuliaji hao hawasababishi madhara

Hakika kazi hiyo wameifanya kwa ustadi mkubwa kwani walifanikiwa 'kuwaweka mifukoni' washambuliaji hao

Wakati Ngoma alipata mwanya wa kufunga bao lililokataliwa na mwamuzi baada ya kumfanyia madhambi Chikupe, nafasi pekee aliyopata Chirwa kwenye kipindi cha kwanza iliokolewa kwa ustadi mkubwa na kipa Klaus Kindoki

Ushindi wa Yanga leo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na umakini wa walinzi hao na wachezaji wote kwa ujumla ambao walikuwa na nidhamu ya hali ya juu katika ulinzi

Licha ya kumiliki mpira kwa muda mwingi, Azam Fc ilikosa mbinu ya kuipenya ngome ya Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’