Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wachezaji wa timu hiyo leo wamekutana na viongozi na kumaliza sintofahamu ya mgogoro uliotokea jana
Zahera amesema sasa wataendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam FC ambao utapigwa Jumatatu, April 29 katika dimba la Uhuru
"Wachezaji leo wamesimulia na viongozi. Wamewaambia mambo yao yote na wamesikilizana, yamemalizika vizuri na mazoezi yanaendelea," amesema
Jana Zahera aliwatahadharisha wachezaji waliogoma kuwa alsingekuwa tayari kuwapokea kama wangeendelea na mgomo huo leo
Hata hivyo leo wachezaji wote walifika mazoezini ambapo jambo la kwanza walionana na uongozi wa Yanga ili kutatua changamoto zinazowakabili
ADVERTISE HERE