Wakongwe Yanga kutoa elimu ya Uchaguzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Apr 2019
Wakongwe Yanga kutoa elimu ya Uchaguzi

Wachezaji wa zamani waliowahi kuitumikia Yanga, kesho Jumamosi wanatarajiwa kufanya kikao Makao Makuu ya klabu hiyo jijini Dar es salaam kujadiliana masuala mbalimbali yanayoihusu Yanga likiwemo suala la uchaguzi

Mwenyekiti wa wachezaji hao Ramadhani Kampila amesema kikao hicho ni mahsusi kwa ajili ya kujadili masuala ya maendelea hasa uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika May 05 2019

"Kesho wachezaji wote wa zamani tutakutana makao makuu ya klabu Jangwani, sababu za kuitisha kikao hiki ni kuzungumzia mambo ya msingi hasa wakati ligi inaelekea ukingoni, pia kupeana elimu kuhusu uchaguzi utakaofanyika," amesema

Kampira amesema Wanayanga hawapaswi kufanya makosa kwenye uchaguzi huo, ni muhimu kuelimishana ili kuhakikisha wanachama wanachagua viongozi ambao wataweza kuitoa Yanga hapa ilipo

"Tumeteseka sana lakini sasa tutapeana mkakati kuhusu viongozi tutakaowachagua kwa sababu tukikosea kwenye uchaguzi huu tutakuwa tumeiweka klabu katika mazingira magumu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’