Inaelezwa sababu kuu ya wachezaji wa Yanga kugomea mazoezi leo ni kushinikiza walipwe madai ya mishahara na fedha za usajili
Baada ya uongozi wa Yanga kubainisha kuwa unakusanya fedha kwa ajili ya kutengeneza timu ya msimu ujao, baadhi ya wachezaji wenye madai wameona kama hawathaminiwi hivyo kuamua kushinikiza walipwe stahiki zao mapema
Wachezaji hao wameutaka uongozi wa Yanga kutumia fedha hizo zilizokusanywa kuwalipa madai yao
Ukiwaondoa Papi Tshishimbi na Kelvin Yondani ambao hawakufika mazoezini leo kutokana na kuwa na ruhusa, wachezaji wengine wote waligoma kufanya mazoezi
Nadhani itakuwa vyema kwa viongozi wa Yanga kuepusha mgogoro huo kwa kuwalipa wachezaji wote wanaodai kwa kutumia fedha hizo ambazo zimechangiwa mpaka sasa
Au njia nyingine wanayoweza kutumia, kama wakati huu hawataki kuzigusa fedha zilizokusanywa, basi waweke hadhani kiasi cha fedha za madai ya wachezaji waliopo ili Wanayanga wafanye zoezi la kuzichangia hizo kwanza
Naamini ukifanyika uhamasishaji mzuri kiasi hicho cha fedha kitapatikana ndani ya muda mfupi