Pengo la Niyonzima linazibika - Lwandamina

habari247 By habari247
•
22 Jun 2017
Pengo la Niyonzima linazibika - Lwandamina
Kocha wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba Afrika ina vipaji vingi anaamini atapata mbadala wa kiungo wa Rwanda, Haruna Niyonzima anayehamia kwa mahasimu, Simba SC.

Kulingana na mahojiano aliyofanya Mzambia huyo na mtandao wa BinZubeiry, Lwandamina amesema kwamba ingawa hajathibitisha kama kweli Niyonzima anakwenda Simba, lakini anaamini mbadala wake atapatikana.

“Mbadala wake anaweza kupatikana na Afrika haiwezi kukosa vipaji. Wakati mwingine familia zinaondokewa na mtu hadi unaanza kufikiria bila fulani mambo hayawezi kwenda,”amesema.

Lakini Lwandamina ameonyesha kushitushwa kidogo na tetesi za mshambuliaji wake, Mzimbabwe Donald Ngoma naye kuwa mbioni kujiunga na Simba.

Yanga jana, kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Charles Boniface Mkwasa imethibitisha kuachana na Nahodha wa Rwanda, Niyonzima baada ya miaka sita na taarifa zinasema anakwenda Simba, lakini pia tetesi zinasema Ngoma naye yuko njia hiyo.

Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia amesema mapema aliagiza wasajiliwe wachezaji watano muhimu, ambao ni beki wa kushoto, beki wa kati, kiungo wa ulinzi, winga wa kushoto na mshambuliaji baada ya kuona mapungufu kikosini msimu uliopita.

“Nimeagiza wasajiliwe mshambuliaji wa nguvu, mfungaji wa magoli, mwenye maamuzi ya haraka, mwenye kujiamini na mpira, anayeweza kutumia miguu yote.

"Pia kiungo mkabaji, beki wa kati anayetumia miguu yote, kiungo wa kushoto na beki wa kushoto,”amesema.

Mwalimu huyo wa zamani wa Zesco United, Lwandamina amesema hakutaja jina la mchezaji hata mmoja, bali alitaja sifa za wachezaji wa kusajiliwa na kwa sababu Katibu Mkwasa ni kocha kitaaluma, anaamini zoezi hilo litakwenda vizuri.

Amesema yeye anatarajiwa kurejea nchini wiki ya kwanza ya Julai kuanza maandalizi ya msimu mpya.

Lwandamina alijiunga na Yanga Novemba mwaka jana kuchukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm baada ya mafanikio yake Zesco akiifikisha Nusu Fainali mwaka jana.

Ameisaidia Yanga kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika msimu mgumu, ambao klabu ilikuwa inakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi iliyosababisha migomo ya mara kwa mara ya wachezaji.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →