Ten awapiga 'dongo' Simba, 'vumilieni ndio ukubwa huo'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Apr 2019
Ten awapiga 'dongo' Simba, 'vumilieni ndio ukubwa huo'

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amewataka mashabiki wa Simba wavumilie 'madongo' wanayovurumishiwa baada ya jana kufumuliwa mabao 4-1 na TP Mazembe na kuondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya robo fainali

Kutupwa nje ya michuano hiyo kwa Simba kuliibua shangwe kubwa miongoni mwa mashabiki wa Yanga na hii inatokana na Simba kutumia mafanikio yao msimu huu 'kuwanyanyasa' watani zao Yanga ambao wanapita katika kipindi kigumu

Ten amesema Yanga na Simba ni watani wa jadi hivyo ni vyema wakavumilia matani wanayokutana nayo mtaani kwani na wao wamekuwa wakifanya hivyo wakati wote ambao Yanga inakumbwa na changamoto

"Ndiyo Sisi na ninyi ni watani na tunataniana kweli hasa timu zetu zinapokosa matokeo," ameandika Ten kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

"Bahati mbaya ni kwamba ninyi mnapenda kutania wenzenu lakini mkitaniwa ninyi 'Nongwa’ mnahamia kwenye kashfa..! Mkikashifiwa nanyi mnaanza kulialia"

"Hongereni kwa hatua mliyofika, muhimu ni kuangalia wapi mmekosea ili mfanikiwe zaidi siku za usoni"

"Wakati sisi tunajiuliza nanyi mjiulize zaidi. Msimvuruge @moodewji ili aendelee kuwabeba..!"

Aidha Ten amewakaribisha Simba kwenye ligi kuu huku akiwatupia 'dongo' kuwa mitandao yao ya simu itakuwa imejaa tayari kwa kufanya miamala

"La huko limeisha, mrudi bongo sasa najua simu zenu zina line mbili mbili yaani full network kama siyo Mpesa basi Tigopesa...!"

Baada ya kutolewa Simba inarejea kwenye ligi ikikumbana na rundo la 'viporo' ambavyo watatakiwa wavimalize ndani ya kipindi cha mwezi mmoja

Katika kipindi hicho Simba wanapaswa kucheza michezo 16 kwani ligi imepangwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa tano ili kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ambayo mwezi Juni inaelekea Misri kushiriki fainali za AFCON 2019

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’