Hii mbeleko ya TFF kwa Simba inakaribia kuchanika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Apr 2019
Hii mbeleko ya TFF kwa Simba inakaribia kuchanika

Leo Simba ilipaswa kucheza na Biashara United. Hata hivyo, TFF imeuahirisha mchezo huo na kuifanya Simba iongeze idadi ya viporo kufikia 11

Simba imeomba kuahirishiwa mchezo huo ili ijiandae na mchezo dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa April 13 Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Huku Simba inaahirishiwa mchezo, lakini kule Congo TP Mazembe kesho itacheza mchezo wa ligi kabla ya kuivaa Simba Jumamosi!

Wakati ligi ikiwa imesalia raundi tano kumalizika, haijafahamika ni utaratibu gani TFF itautumia kuwezesha ligi kumalizika kwa wakati kutokana na klabu ya Simba bado kuwa na michezo mingi ambayo kiuhalisia ratiba yake itakuwa ngumu kupangika kutokana na muda uliobaki

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi mwanzoni mwa msimu, ligi inapaswa kumalizika May 26, ambapo ni kipindi cha mwezi mmoja na siku kidogo

Wakati baadhi ya timu zikisalia na michezo mitano hadi nane, Simba ina michezo 16 ambayo inapaswa ichezwe katika muda huo uliobaki

Kwa muda uliobaki, Simba itapaswa kucheza angalau kila baada ya siku mbili, kinyume na hivyo labda Bodi ya ligi isogeze mbele tarehe ya kumalizika msimu, uamuzi ambao kama utachukuliwa, itafaa upingwe na kila anayelitakia mema soka la Tanzania

TFF wameonyesha upendeleo wa dhahiri kwa Simba na hakika wameweka historia kwa kuifanya timu hiyo icheze ligi bila ya bugudha

Haikuwahi kutokea popote duniani timu moja kurundikiwa michezo 11 ya viporo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’