Zahera awafungulia mlango wanaotaka 'kusepa'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Mar 2019
Zahera awafungulia mlango wanaotaka 'kusepa'

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema amezisikia tetesi zinazowahusu wachezaji wake wanaowaniwa na timu nyingine na ametoa ruhusa kwa mchezaji yeyote anayetaka kuondoka, aondoke

Zahera ambaye yuko Mwanza na kikosi cha Yanga ambacho leo kinatarajiwa kushuka uwanja wa CCM Kirumba kuumana na Alliance Fc katika mchezo wa robo fainali kombe la FA, amesema hana wasiwasi kama wachezaji hao wataondoka kwa kuwa amedhamiria kuisuka upya Yanga kwa ajili ya msimu ujao

Aidha Zahera amesema Yanga ya sasa sio tegemezi, haiwezi kutetereka kama wachezaji hao wataondoka hata leo

"Watu wananipigia simu kuniuliza kuhusu wachezaji wa Yanga hasa Yondani, Tshishimbi, Ajibu na Feisal kutakiwa na timu nyingine."

"Tangu mwanzo wa ligi ukiangalia kuna mechi mingi tulizocheza, angalia mechi ngapi tuilicheza bila Kevin ngapi tulicheza bila Tshishimbi bila Ajibu na Feisal. Kuna mechi tulicheza bila watatu kati yao ndani ya mechi moja na tulishinda," amesema Zahera

"Nikisikia leo Yanga hakuna mchezaji hata mmoja kwenye timu ninaweza kulia lakini mchezaji mmoja akikosa siwezi kukosa usingizi."

"Mchezaji yeyote anayetaka kuondoka anaweza kuondoka, hakuna hata mchezaji mmoja anaweza kuniogopesha kwakuwa timu fulani inamtaka lakini najua msimu ujao wa ligi timu hii itabadilika sana."

"Yanga sio team ya mchezo, Yanga ni timu kubwa na inawachezaji wakubwa. Yanga ina wachezaji wazuri lakini msimu unaokuja nadhani Yanga itakuwa na wachezaji wakubwa saana."

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’