Zahera afunguka maandalizi mchezo dhidi ya Alliance Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Mar 2019
Zahera afunguka maandalizi mchezo dhidi ya Alliance Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kikosi chake kimejiandaa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Alliance Fc ili kutinga nusu fainali ya michuano hiyo

"Tumejiandaa vizuri kupata ushindi mchezo wa kesho. Tunafahamu hautakuwa rahisi lakini nimewaambia wachezaji wangu wajitume ili tuweze kushinda," amesema Zahera

"Tulishasema, michuano hii tumeipa kipaumbele, tukichukua kombe tutajihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao"

Aidha akizungumzia kukosekana kwa baadhi ya wachezaji, Zahera amesema kikosi chake hakitegemei mchezaji mmoja, mchezo wa kesho hautakuwa wa kwanza kwa wachezaji hao kukosekana

"Hii sio mara ya kwanza, Ajib, Ninja hata Gadiel kukosekana. Huko nyuma tumeshacheza bila wao na tukashinda"

"Naamini wachezaji waliopo wataweza kutupatia matokeo mazuri"

Leo jioni Yanga imefanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa CCM Kirumba kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kesho saa kumi kamili jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’