Sanga apita mchujo wa Uenyekiti Kamati ya uongozi, Bodi ya Ligi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2017
Sanga apita mchujo wa Uenyekiti Kamati ya uongozi, Bodi ya Ligi
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha majina ya wagombea wafuatao kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Kamati ya Uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu.

Majina hayo yamepitishwa mara baada ya kuwafanyia usaili uliofanyika Jumapili Septemba 3, mwaka huu kwenye Ukumbi wa TFF, Dar es Salaam.

Uchaguzi Mkuu wa Kamati ya Uongozi wa Bodi ya Ligi utafanyika Oktoba 15, mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi inayotokana na kanuni za uchaguzi za TFF, majina hayo yanapaswa kutangazwa sasa.

Waliopita na majina yao kutangazwa ni Clement Sanga na Hamad Yahya wanaowania uenyekiti wakati Shani Christoms amepitishwa kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Wanaowania nafasi ya ujumbe wako Hamisi Madaki na Ramadhani Mahano. Hawa wamepitishwa kuwania nafasi hizo kutoka Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Pia wamo Almasi Kasongo ambaye anawania nafasi hiyo kupitia Klabu za Ligi Daraja la Kwanza wakati Edgar Chibura anawania nafasi ya ujumbe kupitia Klabu za Ligi Daraja la Pili.

James Bwire yeye hakupitishwa kwa sababu hakufika kwenye usaili.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’