Kufungiwa kwa Buswita ilikuwa maamuzi mengine ya hovyo yaliyofanywa na TFF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Sep 2017
Kufungiwa kwa Buswita ilikuwa maamuzi mengine ya hovyo yaliyofanywa na TFF
Kwanza naipongeza Kamati ya katiba sheria hadhi na wachezaji ya TFF kwa kumtendea haki kiungo Pius Buswita kwa kumruhusu aitumikie Yanga baada ya kulipa fedha alizokuwa amepewa na Simba kwa ajili ya usajili.

Uamuzi huu wa kupongezwa uliofanywa na Kamati leo ulipaswa ufanywe siku ile TFF ilipotangaza kumfungia Buswita.

Kwa mujibu wa sheria za usajili za FIFA, ni kwamba Simba haikuwa imemsajili Buswita bali ilikuwa imemsainisha mkataba wa awali tu pia kumpa pesa za awali (Mil 10) ikiwa na lengo la kumsajili mkataba wake na Mbao FC ukimalizika.

Lakini Yanga ilifuata taratibu zote za usajili ikiwemo kumalizana na klabu yake ya zamani, Mbao FC hivyo kupata vibali halali vya mchezaji huyo kuweza kumtumia kwa miaka miwili kwa mujibu wa mkataba wake.

Maamuzi ya mwanzo hatujui yalifanywa kwa maslahi ya nani, kwani swala hili lilikuwa wazi kabisa.

Mchezaji huyu hakuwemo kwenye usajili wa Simba lakini imeshangaza kuona TFF ikikubali pingamizi kutoka Simba kama vile alikuwa mchezaji wao halali.

Simba ilipaswa kupeleka malalamiko ya kumdai mchezaji huyo hizo pesa walizompa kisha TFF ingeweza kutoa maamuzi kama ilivyofanya leo.

Simba pia ingeweza kwenda hata Mahakami kufungua kesi ya madai dhidi ya Buswita ili alipe pesa zao!

Ni dhahiri maamuzi ya awali yalikuwa na lengo la kumkomesha mchezaji na Yanga iliyomsajili. Kwani maamuzi yalitolewa siku moja kabla Yanga haijacheza na Simba kwenye mchezo wa Ngao ya jamii.

Tukio la kufungiwa Buswita halina tofauti na kilichowatokea Obrey Chirwa na Deus Kaseke.

Walifungiwa halafu baadae wanaambiwa hawana makosa!

TFF iepuke maamuzi ya aina hii yenye kuleta mkanganyiko kwenye jamii wa wadau wa soka hivyo kushusha imani kwao.

Tulitegemea TFF hii mpya iondoe yale yote yaliyokuwa yakilalamikiwa wakati wa utawala wa waliopita lakini inasikitisha kuona hakuna jipya.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’