Ombi la Wanayanga la kutaka uchaguzi linakaribia kukamilika baada ya kuanza maandalizi ya mchakato wa uchaguzi huo
Ili kuhakikisha mchakato unafanikiwa, inaelezwa viongozi waliobaki wanaounda Kamati ya Utendaji ya Yanga wanatarajiwa kujiuzulu nafasi zao wakati wowote ili kufanyike uchaguzi Mkuu ambao ulipaswa kufanyika mwakani
Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga likiongozwa na Mwenyekiti Mh George Mkuchika lilipendekeza kufanyika kwa uchaguzi kamili badala ule wa kujaza nafasi zilizowazi kutokana na muda uliobaki kuelekea uchaguzi Mkuu mwakani
Kamati ya Utendaji ya Yanga imebaki na viongozi wawili tu Samwel Lukumay na Hussein Nyika baada ya hivi karibuni Siza Lymo aliyekuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti na Thobias Lingalangala kujiuzulu nafasi zao
Wadau wa klabu ya Yanga wamependekeza kufanyika kwa uchaguzi haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha timu haivurugi malengo yake
Aidha Yanga inahitaji kuwa na viongozi watakaosimamiwa mchakato wa mabadiliko baada ya kipindi hiki cha mpito