Baada ya kuikabili Alliance Fc jijini Mwanza March 30 katika mchezo wa robo fainali kombe la FA, kikosi cha Yanga kitaelekea mkoani Mtwara kuumana na Ndanda Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara raundi 32
Mchezo huo utapigwa April 03 katika dimba la Nangwanda Sijaona
Yanga itakuwa na siku tatu za kusafiri kutoka Mwanza mpaka mkoani Mtwara kisha kujiandaa na mchezo huo
Ni dhahiri mabingwa hao wa kihistoria Tanzania watalazimika kutumia usafiri wa ndege kwenda sambamba na ratiba hiyo, kama sivyo huenda wakakosa muda wa kufanya maandalizi
Kwani watahitaji angalau siku mbili kusafiri kutoka Mwanza mpaka mkoani Mtwara kama watatumia usafiri wa basi
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera mara kwa mara amekuwa akitoa malalamiko kwa Bodi ya ligi kutokana na ratiba ambayo Yanga imekuwa ikipangiwa huku hali ikiwa tofauti kwa wapinzani wao Simba ambao ratiba imekuwa ikiwabeba mpaka sasa wakiwa na michezo 10 ya viporo
Simba imepangiwa kucheza michezo yake ya viporo wakati ligi itakapokuwa imesimama kupisha michuano ya AFCON ngazi ya vijana itakayopigwa kuanzia April 14-28 katika uwanja wa Taifa na Azam Complex