Buswita ruksa kuitumikia Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Sep 2017
Buswita ruksa kuitumikia Yanga
Kamati ya katiba sheria hadhi na wachezaji ya TFF kupitia kwa Mwenyekiti wake Elias Mwanjala imemaliza utata uliokuwa umegubika kufungiwa kwa kiungo wa Yanga Pius Buswita kwa kumfungulia kiungo huyo aweze kuitumikie Yanga.

Mwanjala amesema baada ya kikao na wajumbe wa kamati hiyo jana Jumanne wamefikia makubaliano ya kumpa ruhusa mchezaji huyo kucheza Yanga.

Mwanjala alisema katika kikao hicho Simba iliwakilishwa na Said Tully na Yanga alikuwa Baraka Dausdedit na wakafikia makubalino ya mchezaji huyo kulipa fedha hizo alizopokea kutoka Simba ili kuanza kuitumikia Yanga.

"Kamati yangu imempa ruksa Buswita kucheza Yanga, lakini kabla ya kuanza kucheza anatakiwa kulipa Sh 10 milioni alizochukua kutoka Simba na kusaini mkataba wa awali," alisema Mwanjala.

"Baada ya kulipa fedha hizo kwa muda wowote atapata ruksa ya kuitumikia Yanga na mwenyewe alikili kuwa kuwa kweli alisaini mkataba na atarudisha fedha za Simba," alisema.

Mjumbe wa kamati ya hiyo Robart Selasela alisema Buswita baada ya kulipa pesa ya Simba watampa onyo kali ila wachezaji wengine kuogopa kufanya jambo kama hilo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’