Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeendelea kujifua kujiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 dhidi ya Uganda
Mchezo huo utapigwa Jumapili, March 24 katika uwanja wa taifa
Nahodha Mbwana Samatta jana aliwasili kukamilisha idadi ya wachezaji wanaosakata kabumbu nje ya nchi
Wachezaji walioitwa Stars wanaocheza soka nje ya nchi ni pamoja na Hassani Kessy (Zambia), Yahya Zayd (Misri), Himid Mao (Misri), Shabani Chilunda (Hispania), Shiza Kichuya (Misri), Simon Msuva (Morocco), Rashidi Mandawa (Botswana), Mbwana Samatta (ubelgiji), Thomas Ulimwengu (Algeria) na Farid Mussa (Hispania)
Stars inahitaji kuifunga Uganda huku pia ikiomba Lesotho isipate ushindi dhidi ya Cape Verde kuweza kukata tiketi ya kucheza fainali za AFCON zitakazofanyika nchini Misri baada ya kusubiri kwa miaka 39