Yanga yakanusha Zahera, Ajib kuondolewa watia saini akaunti CRDB

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Mar 2019
Yanga yakanusha Zahera, Ajib kuondolewa watia saini akaunti CRDB

Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kupuuza taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Kamati ya kuhamasisha uchangiaji iliyochini ya Mh Athony Mavunde imependekeza kuondolewa kwa Kocha Mwinyi Zahera na nahodha Ibrahim Ajib katika miongoni mwa watia saini wa akaunti ya kukusanya michango iliyofunguliwa benki ya CRBD

Msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo amesema hakuna ukweli wowote katika taarifa hiyo na amesisitiza wanaoisambaza ni wenye malengo ya kutaka kuikwamisha Yanga katika mpango wa kujijenga kwa ajili ya msimu ujao

"Hakuna sehemu hata moja kamati imekaa na kuzungumza haya. Huu ni uzushi upuuzwe na apuuzwe aliyeuandika," amesema Ten

"Uongozi kupitia kamati hii ya Mh Mavunde ipo kwenye mikakati mizuri kuhakikisha klabu inavuka kwenye kipindi hiki kifupi wakati ikielekea kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi na mabadiliko mengine"

"Tukumbuke fedha hizi zinakusanywa maaalumu kwa ajili ya usajili na mambo mengine yenye manufaa kwa klabu"

Jana Kamati ya Uhamasishaji ilikutana kwa mara ya kwanza ambapo mpango wa kuchangisha kiasi cha Bil 1.5 uliandaliwa mkakati wa utekelezaji katika kila mkoa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’