Uwanja mkubwa wa soka kujengwa Dodoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2019
Uwanja mkubwa wa soka kujengwa Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu wa Tanzania na Morocco wanaoshughulikia ujenzi wa uwanja wa michezo katika Jiji la Dodoma, unaotarajiwa kujengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI.

Balozi wa Morocco hapa nchini aliyeongoza ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco Mhe. Abdelilah Benryane amesema pamoja na kuzungumzia uhusiano mzuri wa Tanzania na Morocco, wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco hapa nchini mwaka 2016 ikiwemo ujenzi wa Msikiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Jijini Dar es Salaam na kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema uwanja huo utajengwa jirani na eneo la Nanenane kando ya barabara ya Dodoma – Morogoro, utajengwa kwa mfano wa mlima Kilimanjaro na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji kati ya 85,000 na 100,005.

Uwanja huo utakuwa miongoni mwa viwanja vikubwa kabisa barani Afrika ukiupiku uwanja wa Taifa unaochukua mashabiki takribani elfu 60 tu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
45m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’