Mchezo wa jana dhidi ya KMC ulikuwa wa mwisho kwa Yanga uwanja wa Taifa kabla ya kuhamia jijini Mwanza kukamilisha ratiba ya baadhi ya michezo yake ya nyumbani kutokana na kufungwa kwa uwanja huo
Baada ya ushindi huo wa mabao 2-1 dhidi ya KMC, Yanga itaondoka jijini Dar es salaam kwa muda kuahmishia makazi yake Mwanza
Wiki ijayo March 16 Yanga itakuwa mkoani Iringa kuikabili Lipuli Fc ambapo baada ya mchezo huo, mchezo unaofuata utakuwa dhidi ya African Lyon ambao huenda ukawa mchezo wa kwanza wa Yanga kupigwa dimba la CCM Kirumba
Yanga ina michezo mitano nyumbani dhidi ya African Lyon, Kagera Sugar, Mbeya City, Tanzania Prisons na Azam Fc
Uwanja wa Taifa unatarajiwa kufungwa March 24 baada ya mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda, mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019
Viwanja vya Taifa, Uhuru na Azam Complex vinatarajiwa kutumika katika fainali za michuano ya vijana ya AFCON itakayofanyika nchini kuanzia April 14-28
Viwanja hivyo vitafungwa kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati tayari kwa michuano hiyo