Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema alitambua uimara wa KMC hivyo alilazimika kufanya mabadiliko ya mfumo wa uchezaji wa kikosi chake
Kwenye mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, Zahera alianza na mshambuliaji mmoja, Heritier Makambo huku akijaza viungo wengi
"Nilitumia siku mbili kutizama michezo ya KMC, nikabaini hatupaswi kuwapa nafasi ya kumiliki mchezo. KMC kama ilivyokuwa kwa Alliance ni timu ambazo wanacheza pasi kuanzia nyuma," alisema Zahera jana baada ya mchezo
"Kwa kuwa na viungo wengi katikati tulifanikiwa kwa kiasi kikubwa ingawa mara kadhaa tulifanya makosa, moja likiwa bao walilofunga baada ya Ninja kuchelewa kukaba"
"KMC ni timu nzuri, walicheza vizuri ushindi wetu umechangiwa na bahati pia kwani nao walikosa nafasi nyingi"
Yanga ilitawala mchezo huo muda mwingi wa kipindi cha kwanza lakini KMC ilitengeneza nafasi nyingi zaidi kupitia mashambulizi ya kushitukiza
Hata hivyo mabadiliko yaliyofanywa Zahera kwenye kipindi cha pili kwa kuongeza mshambuliaji wa pili (Tambwe) pamoja na Ajib, yaliongeza kasi ya mashambulizi ya Yanga ambapo krosi ya Ajib kwenye dakika ya 67 ilijazwa wavuni na beki wa KMC Ally Ally na kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu