Yanga inahitaji kuunda kitengo cha Uhamasishaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Sep 2017
Yanga inahitaji kuunda kitengo cha Uhamasishaji
Kwanza lazima nipongeze uteuzi wa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha klabu ya Yanga, Dismas Ten ambaye yeye ni mchapakazi hasa.

Kwa kipindi kifupi chini yake tumeona mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa upashanaji Habari kwa klabu ya Yanga.

Yanga sasa inafanya kazi kitaalamu zaidi kuliko ilivyokuwa chini ya Jerry Muro ambaye alifungiwa na TFF msimu uliopita na baadae Yanga kuamua kuachana nae.

Licha ya mafanikio hayo binafsi naona kuna jambo haliko sawa. Binafsi natamani ndani ya ofisi ya Bw, Ten kiundwe kitengo cha uhamasishaji ambacho kitakuwa na kiongozi wake mwenye sifa kama alivyokuwa Murro.

Hakuna ubishi kwenye swala la uhamasishaji Yanga imedorora sana sasa. Tumewapa nafasi wapinzani wetu kutawala kila mahali.

Tumekuwa wanyonge mno. Haji Manara amekosa mtu wa kumchallenge katika kazi yake.

Wakati Yanga inakwenda kupambana na Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii niliushuhdia uwoga mwingi kwa mashabiki wa Yanga kabla ya mchezo huo.

Hii ilitokana na vitisho vya upande wa pili. Wenzetu wanajua umuhimu wa Propaganda, sio jambo la kupuuzwa hata kidogo.

Vyama vya siasa vinaunda mpaka vitengo vya propaganda! Enzi za Jerry Murro mashabiki walimpenda sana kwa sababu alikuwa anafahamu vyema kazi yake.

Murro alisababisha mpaka Manara akawa mpole wakati fulani! Alikuwa na uwezo wa kuwahamasisha mashabiki kupitia vyombo vya habari na wakajitokeza kwa wingi kuishangilia timu.

Kwa hakika Yanga inahitaji mtu wa aina hii. Tuondoe huu unyonge kwa mashabiki wa Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’