Baada ya mapumziko ya siku mbili, kikosi cha Yanga leo kinaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya KMC
Mchezo huo utapigwa Jumapili, March 10 kwenye uwanja wa Taifa
Yanga ilirejea jijini Dar es salaam juzi asubuhi ikitokea Mwanza ambako iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Alliance Fc
Kocha Mwinyi Zahera aliwapa wachezaji mapumziko ya siku mbili ili kurejesha nguvu katika miili yao baada ya kucheza mfululizo
Jumapili Yanga itaikabili KMC ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa
ADVERTISE HERE