Jana uongozi wa Yanga ulitoa taarifa yake ya kwanza iliyobainisha kiasi cha fedha zilizopatikana katika kampeni ya kuichangia timu hiyo iliyoanzishwa mapema mwezi huu
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh alisema mpaka jana, jumla Tsh Mil 21 zilikuwa zimechangishwa kupitia mitandao ya MPESA, TIGOPESA na Akaunti ya CRDB
Hata hivyo Hafidh alisema mwitikio wa uchangiaji bado ni mdogo sana hivyo kuwataka wanachama na mashabiki wa Yanga waendee kujitoa kuhakikisha malengo yanafikiwa
Yanga iliweka malengo ya kukusanya Tsh Bil 12.5
Mipango ya Yanga hasa kwa msimu ujao inategemea zaidi na ushirikiano kutoka kwa wadau wake hasa ikizingatiwa timu hiyo kwa sasa inapita katika kipindi kigumu
Kocha Mwinyi Zahera ndiye aliyetoa wazo la kuwashirikisha Wana Yanga wote ili timu hiyo ipate uwezo wa kifedha haraka
Kiasi hicho cha pesa kinatarajiwa kutumika kufanya usajili mwishoni mwa msimu pamoja na kuboresha maeneo mbalimbali likiwemo kumalizia ukarabati wa uwanja wa Yanga
Hata hivyo haya yatakamilika kama Wana Jangwani wote watajitoa kuichangia timu yao