Winga wa Yanga Mrisho Ngasa jana alijibu kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye siku chache zilizopita alimkosoa kuwa ameisha na ni vyema akatafuta shughuli nyingine ya kufanya
Ngasa alisema kauli hiyo haimsumbui kwa sababu anaamini ukiwa mtu maarufu inakupasa uwe tayari kusimangwa, kutukana na kusemwa vibaya
"Kwa sababu kwetu tumefundishwa mkubwa hakosei kwa hiyo mimi siwezi kumlaumu kwa sababu yeye kipaji chake ni kuongea na mimi ni changu ni kucheza mpira. Na pia katika mpira kuna kutukanwa kwa hiyo ukiwa staa lazima uwe tayari kwa lolote," alisema Ngasa
"Tunamshukuru mungu, sisi wabaya tunaongoza ligi, lakini pengine tulipaswa tuwe nafasi ya kumi na kushuka chini"
"Sisi tunamshukuru Mungu, kwani kamuweka (Muro) katika nafasi alipo si kimakosa. Yeye ni Mheshimiwa na tunaamini waheshimiwa hawakosei"
Katika hatua nyingine, Muro amewaomba radhi kocha Mwinyi Zahera, Ngasa, Boban na Wana Yanga kufuatia kauli yake aliyotoa hapo juzi
