Stars inachuana na Botswana leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
2 Sep 2017
Stars inachuana na Botswana leo
Timu ya Taifa ya Tanzania leo itashuka dimba la Uhuru jijini Dar es salaam kupambana na Botswana katika mchezo wa kirafiki ambao uko kwenye kalenda ya FIFA.

Katika mchezo huo, mwamuzi wa kati anatarajiwa kuwa Elly Sasii akisaidiwa na Soud Lillah (Line 1) na Frank Komba (Line 2) wakati mwamuzi wa akiba (Forth Official) atakuwa Israel Nkongo.

Jana Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, alisema: “Kikosi chetu kipo tayari kwa mchezo huu ambao kwetu
ni muhimu kwa maana mbili, moja ni kujiandaa na michezo ijayo ya kufuzu Afcon, lakini pili ni kutafuta nafasi ya kupanda kwenye viwango vya Fifa.

“Kikubwa Watanzania wajitokeze uwanjani kutusapoti kwani vijana wamenihakikishia kwamba wana uwezo wa kushinda mchezo huu.”

Kwa upande wake Kocha wa Botswana, Major David Bright, alisema: “Tumekuja lakini bado tuna uchovu wa safari, lakini tunatarajia kuwa na mchezo mzuri dhidi ya Tanzania kwani hii si mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana.

“Nimepewa kikosi hiki hivi karibuni, lakini nimejaribu kuchukua wachezaji wale wazoefu na naamini tutafanya vizuri. Mechi hii ni kipimo kwetu kwa ajili ya kujiandaa na mechi za kufuzu Afcon.”

Viingilio vya mtanange huo, Mzunguuko Tsh 5,000 huku VIP ikiwa Tsh 10,000
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →