Wambura apandishwa kizimbani, atangaza kuachana na soka

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Feb 2019
Wambura apandishwa kizimbani, atangaza kuachana na soka

Mapema leo aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Michael Wambura kupitia kwa Wakili wake Emmanuel Augustine Muga alitangaza rasmi kuachana na masuala ya uongozi wa mpira wa miguu huku akitangaza kuondoa kesi zote zilizokuwa Mahakamani baina yake na TFF

Muda mfupi baada ya Wakili wake kutoa taarifa hiyo, Wambura alipandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam akikabiliwa na Mashitaka 17 yakiwemo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na kutakatisha fedha

Kesi hiyo namba 10/2019 itatajwa tena Februari 14 2019 na Wambura amepelekwa rumande baada ya kukosa dhamana

Hivi karibuni, baada ya kushinda Rufaa ya kuondolewa wadhifa wake wa Makamu wa Rais wa TFF, Shirikisho la mpira la mpira duniani (FIFA) lilikazia Maamuzi ya TFF ya kumfungia maisha kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu

Hata hivyo Wambura alikwenda Mahakamani kupinga hukumu hiyo akikazia uamuzi wa Mahakama Kuu kumrejesha katika wadhifa wake kabla ya leo kuamua kufuta kesi na kuachana na masuala ya uongozi wa soka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’