Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameendelea kukinoa kikosi chake tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa kesho Jumapili katika dimba la Mkwakwani
Leo asubuhi Yanga ilijifua katika uwanja huo wa Mkwakwani
Katika mazoezi hayo Zahera alisisitiza umuhimu wa wachezaji wake kujaribu kufunga mabao wakiwa nje ya 18
Yanga imekuwa ikifunga mabao yake mengi kupitia mipira ya krosi lakini kwa michezo ya hivi karibuni imekumbana na changamoto ya mabao hayo kukataliwa na waamuzi kwa wafungaji kudhaniwa wameotea
Zahera amewapa msisitizo wachezaji wake kujaribu kupiga mashuti wakiwa nje ya 18 wapatapo nafasi
Baada ya kukosa ushindi kwenye michezo mitatu ya ligi iliyopita, Yanga inahitaji sana ushindi katika mchezo wa kesho