Hakuna asiyejua ugumu wa michezo ya mikoani hasa katika mzunguuko huu wa pili wakati ambao baadhi ya timu zinapigana kupata pointi zijinusuru na kuteremke daraja
Nyakati kama hivi alama moja inakuwa na umuhimu mkubwa kuliko inavyofikiriwa
Yanga bado inanufaika kwa kujikusanyia alama nyingi kibindoni ikiendelea kuongoza ligi na alama zake 55
Ndio, Yanga tayari inazo pointi zake kibindoni, sio sawa na wale ambao wanahesabu pointi ambazo bado sio zao
Mpaka sasa wanahitaji kucheza dakika 720 kuweza kukipata kile ambacho Yanga tayari inacho mkononi
Baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania, Yanga itarejea jijini Dar es salaam kuwasubiri 'vibonde wa Kimataifa'
Sare hizi mbili mfululizo zimeipa Yanga sababu 100 za kushinda mchezo wa Februari 16
ADVERTISE HERE