Wananchi Singida waisubiri Yanga mpaka usiku, waipokea kwa shangwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Feb 2019
Wananchi Singida waisubiri Yanga mpaka usiku, waipokea kwa shangwe

Jana usiku kikosi cha Yanga kiliwasili salama mkoani Singida wakitokea Tanga tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Songida United utakaopigwa kesho Jumatatu katika uwanja wa Namfua

Licha ya timu hiyo kuchelewa kuingia Singida, umati mkubwa wa Wananchi waliendelea kuwasubiri vinara hao wa ligi kuu na shangwe zikatawala baada ya basi lililobeba wachezaji na viongozi wa Yanga kuwasili

Leo jioni Yanga inatarajiwa kujifua kwenye dimba la Namfua tayari kuwakabili Singida United, wakisaka ushindi wao wa kwanza dhidi ya walima alizeti hao katika dimba la Namfua

Msimu uliopita timu hizo zilikutana mara mbili katika dimba hilo na matokeo ya michezo yote yalikuwa sare ya bao 1-1. Singida United ikishinda kwa matuta katika mchezo wa kombe la FA

Msimu huu Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza ambao ulipigwa katika dimba la Taifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’