Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe jana alipata majeraha usoni baada ya kugongana na mlinda lango wa Biashara United Nurdine Balora
Hali ya mshambuliaji huyo mwenye mabao sita kwenye ligi na manne kwenye michuano ya kombe la FA, inaendelea vizuri
Huenda akaukosa mchezo wa keshokutwa dhidi ya Coastal Union kutokana na majeraha hayo
Tambwe ndiye aliyefunga bao la kwanza la Yanga kwa mkwaju wa penati jana dhidi ya Biashara United katika mchezo ambao dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 na kisha Yanga kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4
ADVERTISE HERE