Zahera apania kuisimamisha Simba Februari 16

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jan 2019
Zahera apania kuisimamisha Simba Februari 16

Kwa takribani misimu mitatu mfululizo Yanga imeshindwa kuwafunga watani zao Simba katika michuano yote waliyokutana.

Hans van Pluijm ndiye kocha wa mwisho kuifunga Simba wakati akiiongoza Yanga msimu wa 2015/16

George Lwandamina ambaye alichukua nafasi ya Pluijm hakuweza kuifunga Simba katika kipindi cha msimu mmoja na nusu aliokuwepo Jangwani

Chini ya Lwandamina Yanga ilipata sare mbili na kufungwa michezo miwili kwenye ligi

Kocha wa sasa wa Yanga Mwinyi Zahera yeye ameanza kwa sare kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza msimu huu

Mchezo unaofuata baina ya timu hizo unatarajiwa kupigwa Februari 16 2019

Zahera amesema mchezo huo utakuwa tofauti sana na mchezo wa kwanza

Zahera aliyejipambanua kwa kuwa muwazi, amesema mchezo wa mzunguuko wa kwanza kikosi chake hakikuwa vizuri, alilazimika kutumia mbinu ya kijuhami zaidi kwani kama angecheza mpira wa kufunguka, angeweza kupoteza mchezo huo

Sasa hali ni tofauti, kikosi cha Yanga kimeimarika. Yanga inaongoza ligi kwa tofauti ya alama sita dhidi ya Azam FC huku Simba yenye viporo vingi ikishika nafasi ya nne ikiwa na alama 33

Lakini kinachompa kiburi zaidi Zahera ni ujio wa wachezaji wawili, mkongwe Haruna Moshi 'Boban' na Mohammed Issa 'Banka'

Boban aliyesajiliwa na Yanga wakati wa usajili wa dirisha dogo akitokea African Lyon, ameanza kuzoeana na wenzake wakati Banka ambaye sasa anajifua na kikosi cha Yanga ataanza kuonekana rasmi dimbani Februari 09 baada ya adhabu yake kumalizika Februari 08

Zahera amesema uwepo wa wachezaji hao umeongeza nguvu katika kikosi chake, anaimani watasaidia kuisimamisha Simba watakapokutana Februari 16.

"Mechi haiwezi kuwa kama ilivyokuwa mzunguko wa kwanza, nina uhakika Boban na Banka watatusaidia sana tutakapokutana," amesema

"Ukiangalia tu wanavyofanya mazoezi na namna walivyoongeza nguvu kikosini, ninaamini tunaweza kushinda mechi hiyo"

Zahera amemsifia kiungo Mohammed Issa kuwa ni aina ya wachezaji aliowahitaji katika timu yake na anaamini kiungo huyo atakapomaliza adhabu yake ataisaidia sana Yanga

Ukiachana na wachezaji hao, Yanga inajivunia uwepo wa viungo Feisal Salum na nahodha Ibrahim Ajib, washambuliaji Amissi Tambwe na Heritier Makambo ambao ushirikiano wao umeanza kuwa na faida kwa mabingwa hao wa kihistoria

Ajib hakun'gara katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza, lakini hakuna shaka Februari 16 sasa akiwa nahodha, atakuwa chachu ya mafanikio ya Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’