Zahera apiga hesabu za mataji mawili msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jan 2019
Zahera apiga hesabu za mataji mawili msimu huu

Yanga itaingia kambini kesho Jumanne kujiandaa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Biashara United utakaopigwa siku ya Alhamisi, Januari 31 kwenye dimba la Taifa

Vinara hao wa ligi kuu wanapiga hesabu kali kuhakikisha wanatwaa mataji mawili, yaani ligi na kombe la FA (ASFC)

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameweka wazi kuwa malengo ya timu yake sasa ni kushinda mataji hayo mawili baada ya kutolewa mapema katika michuano ya SportPesa Cup iliyomalizika jana kwa K. Sharks kutawazwa mabingwa

Zahera amesema wachezaji wake wanafahamu malengo hayo na ndio maana wamekuwa wakijituma kuhakikisha wanafikia matarajio ya Wana Jangwani

Baada ya mchezo wa kombe la FA, Yanga itaelekea mkoani Tanga kuikabili Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa Februari 03

Zahera amesema kwa sasa hesabu zake amezielekeza kombe la FA, baada ya mchezo dhidi ya Biashara Fc watahamisha nguvu zao kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Union.

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’